Swali: Nimechukuliwa katika chuo kikuu cha Kiislamu. Baba yangu ananikatalia kwenda al-Madiynah kwa sababu anaona kwamba kusoma masomo ya kidini ni kupoteza wakati. Ananitisha ya kwamba nikienda basi atajitenga mbali na mimi. Nifanye nini na baba yangu amabye haswali na wala hajali kabisa mambo ya kidini?

Jibu: Usimtii. Nenda ukasome na ujifunze. Amekuamrisha maasi na hakukuamrisha utiifu:

“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”[1]

[1] al-Bukhaariy (7258) na Muslim (1840).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (71) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah26-07-1438h%20-%20Copy.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2017