Swali: Nikiwa ni mwenye kujiheshimu kwa vazi la Kiislamu nyumbani na wala siachi (kuvaa) Khimaar (shela, ushungi) kichwani mwangu. Je, inajuzu kwangu kukaa na watoto wa kiume wa ami na shangazi yangu na mfano wao ikiwa sote ni wanaume na wanawake twakaa sehemu moja?

Jibu: Hakuna ubaya kukaa na watoto wa ami na shangazi pamoja na kuwa na heshima, kujisitiri na kuvaa Hijaab. Hata uso, ni ´Awrah kwa kauli ya sahihi. Ni wajibu fuunika na kichwa, hivyo viwili ni aula zaidi atapokaa na ndugu zake; watoto wa shangazi, mjomba au jirani yake kwa mipaka mizuri ya kidini isiyokuwa na neno ndani yake. Pamoja na kujisitiri, kuvaa Hijaab na wala kutoonesha kitu katika hivyo; si uso wala kingine chochote, hakuna ubaya kwa hilo. Na wala haitoshi kufunika kichwa, bali ni wajibu kufunika uso pia. Mwanamke anatakiwa kujiheshimu na kujiweka mbali na sababu zinazopelekea katika fitina; (asichukulie sahali) si pamoja na watoto wa shangazi yake, mjomba wake wala wasiokuwa wao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb (770)
  • Imechapishwa: 16/03/2018