Ndugu kuoana kuna maradhi – kampeni za makafiri

Swali: Kuna wengi wanakataa kuoa ndugu kwa kutumia hoja ya kwamba jambo hilo linaweza kuleta maradhi. Ni upi usahihi wa madai haya?

Jibu: Hili halijuzu. Haya yanatoka umagharibini na sio katika Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alioa katika ndugu zake na akamuozesha msichana wake Faatwimah kwa ´Aliy bin Abiy Twaalib. Maswahabah walioa ndugu zao na wala Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwakataza hilo. Hii ni fikra ya kimagharibi. Lililo la dhahiri ni kwamba wanakusudia kwa hilo kupunguza kizazi kwa waislamu. Wanasema “Zaeni watoto kadhaa tu”, “Zaeni uzazi wa mpango”, “Jiepusheni kuoa ndugu”, yote haya ni kampeni za kutooa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mhdr-09-11-1432.mp3
  • Imechapishwa: 24/09/2020