Ndoa ya waliozini


Swali: Kuna mtu kazini na mwanamke kisha akambebesha mimba na sasa mwanaume huyo anataka kumuoa, pamoja na kuwa katubia kwa Allaah. Je, imeshurutishwa mpaka ajifungue au haikushurutishwa?

Jibu: Muislamu haijuzu kwake kuoa/kuolewa na mzinifu. Isipokuwa kwa masharti mawili:

1- Sharti ya kwanza atubu Tawbah ya sahihi ya kuacha Zinaa; aiache, ajute kwa hilo na aazimie kutorudi kufanya hivyo.

2- Sharti ya pili ni lazima kwake yeye mwanamke kukaa eda, pengine akawa amepata mimba kwa Zinaa hiyo. Ni lazima akae eda kwa kupata hedhi mara tatu. Ikiwa yatatimia masharti haya mawili, inajuzu kuoana. Ama maadamu hajatubia, haijuzu kuolewa nae. Kutokana na Kauli Yake (Ta´ala):

الزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ ۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ

“Mzinifu mwanamme hafungamani (hafungi Nikaah) isipokuwa na mzinifu mwanamke au mshirikina mwanamke; na mzinifu mwanamke hafungamani naye (haolewi na yeyote) isipokuwa na mzinifu mwanamme au mshirikina mwanamke. Na imeharamishwa hivyo kwa Waumini.” (24:03)

Huyu haijuzu kuolewa naye. Na mimba hii sio ya kwake [baba], hatokuwa mtoto wake. Na pengine ikawa ya mtu mwengine maadamu mwanamke anazini. Unajuaje kama huyu ni mtoto wako? Hili halijuzu. Mtoto wa Zinaa huu haendi kwa baba, isipokuwa anaenda kwa mama yake tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/2948
  • Imechapishwa: 11/01/2018