Ndoa ya siri


Je, inajuzu kufanya ndoa ya siri? Suala hili linagawiwa sehemu mbili:

1- Mwanaume, mwanamke na walii wake wanakubaliana ya kwamba inatakiwa kuwa siri. Baada ya hapo ndoa ikafanywa kwa mashahidi na masharti yaliyotimia. Kisha wakakubaliana ya kwamba kuifanya ndoa kuwa ya siri. Baadhi ya wanachuoni wanasema kuwa ndoa hii si sahihi. Maoni yaliyotangaa katika madhehebu ya Ahmad wanaonelea ya kwamba ndoa haiachi kuwa sahihi kwa ajili tu ya sababu hii.

2- Wanaficha hilo bila ya makubaliano. Bila ya shaka hili halikuwekwa katika Shari´ah. Lililowekwa ni kutanganza ndoa kutokana na maamrisho ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[1]. Hali kadhalika tendo hili linawashaji´isha wengine kuoa.

[1] at-Tirmidhiy (1089) na Ibn Maajah (1895).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam min al-Qur-aan al-Kariym (2/180-181)
  • Imechapishwa: 20/09/2020