Ndoa ya mwanamke kajioza mwenyewe bila walii

Swali 240: Unasemaje juu ya mwanamke ambaye amejiozesha mwenyewe kwa hoja kwamba madhehebu yake ni Hanafiyyah?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza mwanamke kujioza mwenyewe na akasema:

“Mwanamke mzinifu ni yule mwenye kujioza mwenyewe.”

Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ndoa haisihi isipokuwa kwa walii.”

Watu hao wanatumia dalili kwa Hadiyth inayosema:

“Mtumzima ana haki juu ya nafsi yake.”

Lakini maana yake ni kwamba ana haki ya kujichagulia mwenyewe, ana haki ya kuyathibitisha yale anayoambiwa au ana haki ya kuyakatazaa. Maana yake si kwamba ajioze mwenyewe. Lau kusingelipokelewa isipokuwa Hadiyth hii ya Abu Muusa al-Ash´ariy tu [basi ingetosha] ambayo ipo katika “as-Sunan”:

“Ndoa haisihi isipokuwa kwa walii.”

Kwa hiyo likitokea jambo kama hilo basi ndoa kuanzia mwanzo wake imejengwa juu ya madhehebu ya ki-Hanafiy na hivyo ndoa hiyo ina shubuha.

Wakipata watoto basi watoto hao ni wenye kumfuata baba yao. Walii anatakiwa kuwaomba kuifanya upya ndoa yao na himdi zote anastahiki Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ndoa haisihi isipokuwa kwa walii.”

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 460
  • Imechapishwa: 30/10/2019