Ndoa ya kaka aliyemuozesha dada yake bila idhini ya baba

Swali 692: Kaka yake alimfungisha ndoa na baadaye baba yake na mwanamke akaafiki.  Tufanye nini ikiwa tunataka kusahihisha ndoa hii huko baadaye?

Jibu: Mwanamke akifungishwa ndoa na kaka yake pasi na uwakala/idhini kutoka kwa baba yake, ndoa hiyo haisihi. Haijalishi kitu hata kama baadaye baba yake ataafiki. Ikiwa watataka kusahihisha ndoa hiyo basi baba yake mwenyewe ndiye amfungishe ndoa mpya au anaweza vilevile kuwakilisha mtu wa kumfungisha ndoa. Ni mamoja akamuwakilisha kaka yake au mwengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 268
  • Imechapishwa: 26/08/2019