Swali: Mwanamke huyu alikuwa ni mnaswara ambapo akaingia ndani ya Uislamu. Lakini mume wake akabaki kwenye unaswara wake. Je, inafaa kwake kubaki pamoja naye? Je, kuna muda maalum uliowekwa?

Jibu: Mwanamke akisilimu na mume wake asisilimu, basi atakaa na kusubiri muda wa eda. Akisilimu kabla ya eda kuisha basi ataendelea kuwa mume wake. Asiposilimu isipokuwa baada ya eda yake ametengana naye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (99) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/%D8%A5%D8%BA%D8%A7%D8%AB%D8%A9%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%D9%81%D8%A7%D9%86-10-07-1440%D9%87%D9%80_0.mp3
  • Imechapishwa: 22/07/2019