Swali: Kuna mtu kamjamii mwanamke wake ambaye alikuwa anataka kumchumbia kabla ya kufunga ndoa, akambebesha mimba akamwambia hilo walii wa mwanamke. Wakawa wamefunga ndoa kisha Allaah akawaruzuku mtoto. Ipi hukumu ya mtoto huu Kishari´ah kwa kuzingatia kuwa baba amekubali ni wake?

Jibu: Mtoto huyu ni wa zinaa. Kwa kuwa kufanya nae jimaa kabla ya kutimia kwa ndoa, ni jambo ovu na zinaa. Hatonasibishwa nae na wala hatokuwa mtoto wake, isipokuwa atanasibishwa kwa mama yake, au atanasibishwa kwa ´Abdullaah, ´Abdul-Latwiyf, ´Abdul-Maalik kwa minajili ya kumsitiri katika mustakabali. Muhimu ni kwamba, hatonasibishwa kwa baba yake kwa kuwa ni mtoto wa zinaa, lakini badala yake atanasibishwa kwa mama yake. Ni juu yao wote kufanya tawbah. Ni juu ya mwanaume na mwanamke watubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na wafunge ndoa upya, kwa kuwa ndoa ilifanywa katika hali ya ujauzito wa zinaa. La wajibu ni wafunge ndoa upya, baada ya kujifungua. Awafungishe ndoa walii wa mwanamke, baada ya wote wawili kutubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=DhG-DF3140U
  • Imechapishwa: 06/05/2021