Ndoa inatakiwa kuwafanya wanandoa kutafuta elimu

Swali: Ni ipi nasaha yako kwa yule ambaye ndoa inamzuia kutafuta elimu?

Jibu: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hakuweka ndoa ili ikuzuie na matendo mazuri, kutafuta elimu na kulingania katika dini ya Allaah. Baadhi ya watu wanapooa ndoa inawazuia na matendo mazuri mengi. Hii sio sababu ambayo Allaah ameweka ndoa kwa ajili yake. Ameiweka ili wewe na mke wako mzidishe kufanya matendo mazuri, kufanya Da´wah, du´aa, ´ibaadah na kutafuta elimu. Ndoa ni neema. Mtu anapopata neema mpya basi amshukuru Allaah kwayo. Lakini ikiwa unarudi nyuma kila wakati unapopata neema maana yake ni kwamba humshukuru. Allaah amesema:

لَئِن شَكَرْتُمْ لَأَزِيدَنَّكُمْ ۖ وَلَئِن كَفَرْتُمْ إِنَّ عَذَابِي لَشَدِيدٌ

“Mkishukuru, bila shaka Nitakuzidishieni  na mkikufuru, basi hakika adhabu Yangu ni kali.” (14:07)

Izungumzishe nafsi yako ya kwamba kila wakati kunapokuja neema mpya basi majukumu na shukurani vinazidi. Hutakiwi kurudi nyuma.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/index.php?article_id=2697
  • Imechapishwa: 20/09/2020