Ndoa iliofungwa pasina walii wa mwanamke

Swali: Maswali haya mawili yanahusiana na sura moja. Mwanaume amemuoa mwanamke pasina kuwa na walii. Na ndoa hii imeshapita miaka mingi. Na mwanamke huyu amekwishazaa na mwanaume huyu. Je, ndoa hii ni batili au wafanye nini?

Jibu: Ndoa hii ni yenye kuharibika na sio batili. Ni wajibu kwao kwenda kwa hakimu mpaka aweze kuisitisha ndoa hii na kuifunga upya. Ama watoto waliopata pamoja, ni watoto wa Kishari´ah kwa utata.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/4030
  • Imechapishwa: 22/09/2020