Swali: Sisi katika maeneo yetu tuko na darsa za kielimu msikitini. Zinaendeshwa na baadhi ya Mashaykh na wanafunzi wanaofuata Qur-aan na Sunnah. Tuliwaomba hawa mashaykh kufanya darsa zao sehemu ya mapumziko kila mwezi. Lengo ni wakusanyike watafutaji elimu sehemu hii ya mapumziko kila na wanazidi kuvutiwa. Mmoja katika mwanafunzi akanikatalia jambo hili kwa hoja kuwa ni kuihama misikiti na kwamba njia hizi za mapumziko na kupafanyia darsa za kielimu ni njia za Hizbiyyuun. Wasemaje kuhusiana na maneno haya?

Jibu: Ndio, maneno haya yana maana. Darsa zinakuwa misikitini. Ama nasaha na mawaidha hakuna ubaya ukaenda sehemu za mapumziko ukawaweka sawa na kuwakumbusha. Ama darsa sehemu kama hizi badala ya misikitini, hili halifai. Ana maanisha kuwa Hizbiyyuun ni wasiri. Hawajidhihirishi misikitini. Wanaenda sehemu za mapumziko au sehemu za kujificha. Hawafanyi haya misikitini. Kwa kuwa watu watawakataza mambo haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/9364 Tarehe: 1431-06-11/2010-05-24
  • Imechapishwa: 09/04/2022