Faida ya sita: Hadiyth inathibitisha kwamba wanachuoni wanatakiwa kuheshimiwa na kutowafanyia maskhara na mzaha. Mnafiki huyu alisema:

“Hatujawahi kuona mfano wa wanachuoni wetu hawa ambao ni waroho sana, waongo na waoga wakati wa mapambano.”

akilenga wanachuoni. Wanachuoni ndio warithi wa Mitume na wao ndio viigizo vya Ummah. Wakitukanywa wanachuoni kunapelekea ghasia katika jamii ya Kiislamu, thamani ya wanachuoni inapungua na kunafanywa wakadhaniwa vibaya.

Tunasikia na tunasoma kutoka kwa walinganizi waovu wanaowaita wanachuoni kwa mfano ni wanachuoni wa hedhi na wanachuoni wa nifasi, wanachuoni wa watawala na wanachuoni wa nyumbu ya mtawala. Maneno kama haya yanaingia katika mlango huu. Hakuna kilichomfanya mtenda dhambi huyu mbaya kusema hivo isipokuwa tu ni kwa sababu hawaafikiani naye katika mfumo wake uliopinda. Haijuzu hata kumtukana muislamu wa kawaida, kwa sababu muislamu ana heshima yake. Kusemwe nini juu ya watawala na wanachuoni wa waislamu? Ni lazima kutahadhari kutokamana na mambo haya, kuchunga ulimi, kupiganisha kutengeneza na kumnasihi yule anayefanya kosa hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 533-543
  • Imechapishwa: 04/09/2019