Swali: Kuna dalili ya wazi yenye kuharamisha kupiga makofi? Inajuzu kupiga makofi kwa ajili ya kuwashaji´isha wanafunzi kwenye madrasah?

Jibu: Kupiga makofi ni katika ada ya makafiri. Sisi hatujifananishi na makafiri. Hii ni sababu moja. Sababu nyingine ni kuwa wanawake ndio wenye kupiga makofi. Wanawake ndio wenye kupiga makofi na wanaume wanasema “Subhaan Allaah”, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kupiga makofi ni katika sifa maalum za wanawake. Haifai kwetu kupiga makofi. Sisi si wanawake mpaka tupige makofi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir%20ayat-03-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/06/2020