Sababu ya kupatikana kasoro kwa watu wengi ni kule kupingana kwao na Maneno ya Allaah na Mtume Wake na badala yake wakajishughulisha na maneno ya wagiriki na maoni mbali mbali. Kwa ajili hiyo ndio maana wameitwa kuwa ni “wanafalsafa”, Ahl-ul-Kalaam. Wameitwa hivi kwa sababu hawakuleta elimu ambayo haikuwa yenye kujulikana. Ni kwa sababu wameleta ziada ya maneno yasiyofidisha kitu. Wanayagonga [maandiko ya Kishari´ah] kwa kutumia vipimo [Qiyaas] na ukiongezea juu yake hisia zenye kujulikana.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/272)
  • Imechapishwa: 21/05/2020