Ndio maana usiku wa Qadr ukafichwa

Zirr bin Hubaysh amesema:

“Nilimsikia Ubayy bin Ka´b akisema: “´Abdullaah bin Mas´uud amesema kwamba yule atakayeswali mwaka mzima basi ataupata usiku wa Qadr. Ndipo Ubayy (Radhiya Allaahu ´anh) akasema: “Allaah amrehemu kwa sababu hakutaka watu wabweteke. Ninaapa kwa Mungu wa haki kwamba uko katika Ramadhaan. Ninaapa kwa Allaah pia najua ni usiku gani unatokea! Ule ambao Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametuamrisha kuswali ilikuwa usiku wa tarehe ishirini na saba. Alama yake ni kwamba jua linakuwa halina miale ya kuchoma.”[1]

Kwa jumla ni kwamba Allaah ameuficha usiku huu juu ya Ummah huu ili wajipinde katika ´ibaadah katika zile nyusiku za Ramadhaan hali ya kuwa na matumaini ya kuupata. Ni kama ambavo ameificha saa ya kujibiwa du´aa katika ile siku ya ijumaa, ile swalah ya katikati katika vile vipindi vitano vya swalah, jina Lake tukufu miongoni mwa majina mengine na radhi Zake kwenye utiifu na hasira Zake katika maasi ili wajiepushe na yote hayo. Vilevile ameficha wakati ambapo Qiyaamah kitasimama ili wapate kujipinda kwa matendo mema kwa ajili ya kujichunga kusimama kwake.

[1] Muslim na wengineo. Imetajwa katika ”Swahiyh Abiy Daawuud” (1247).

  • Mhusika: Imaam al-Husayn bin Mas´uud al-Baghawiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim-ut-Tanziyl (4/511)
  • Imechapishwa: 15/05/2020