Ndio maana rekodi ya kanda za video ni ´ibaadah inayofaa

Ikiwa doli za wasichana zinajuzu kwa lengo la mafunzo, basi picha muhimu zaidi ni aula zaidi kuwa zinajuzu. Mfano wa picha hizo ni kama zile zinzotumiwa katika vitambulisho, pasipoti na venginevyo vinavyonufaisha Ummah.

Vivyo hivyo nasema kuhusu kurekodi video camera. Endapo kifaa hichi kitatumiwa kuwafunza waislamu baadhi ya ´ibaadah ambazo hawawezi kujifunza nazo kwa njia ya kusikia peke yake, lakini wanaweza kujifunza nazo kupitia njia ya kuona. Kama kungelikuweko nchi ya Kiislamu kikweli ambayo inawafunza waislamu kuhiji; namna ya kufanya Twawaaf kwenye Ka´bah, ni wapi wataanza kufanya Twawaaf, ni vipi wanatakiwa kuligeukia lile jiwe jeusi, ni wapi wanatakiwa kwenda baada ya Twawaaf, nini wanachotakiwa kufanya kukiwa kuna msongamano na kadhalika. Kwa njia hiyo mahujaji wanajifunza hajj ilihali wamo majumbani mwao. Hali kadhalika inahusiana na swalah:

“Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”

Waislamu wengi hawajui namna ya swalah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hata wale wanaojiita kuwa ni wanachuoni katika Fiqh na madaktari hawajui ni namna gani aliswali. Wote wamejifunza swalah kwa mujibu wa madhehebu fulani. Ahnaaf wanaswali kwa kuweka mikono chini ya kitovu, Maalikiyyah namna hii, Shaafi´iyyah namna hii.. Ni wachache mno wanaoweka mikono juu ya kifua kama alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Baadhi wananyanyua mikono yao wakati wa Takbiyrat-ul-Ihraam. Wengine wanafanya hivo wakati wa kwenda katika Rukuu´. Ni kipi chenye manufaa zaidi? Kurekodi kanda ya video kuhusu swalah na hajj ya Mtume ni jambo linalonufaisha ulimwengu mzima wa Kiislamu au doli za ´Aaishah? Ikiwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alihalalisha hayo, basi haya yana haki zaidi kuwa halali.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (834) Muda: 53:50
  • Imechapishwa: 11/01/2021