Mtu huyu – Sayyid Qutwub – na wafuasi wake ndio fitina ya wakati huu. Ndio fitina kubwa ya leo kwa sababu inadai mfumo wa Salaf-us-Swaalih.

Ndugu! Jihadharini na wao! Wana utatizi, udanganyifu, vitimbi, hila na uongo ambao unajua Allaah Peke Yake. Kazi yao yote iko kwa ajili ya kuwawinda vijana. Hawajali kuwalingania manaswara, mayahudi, Rawaafidhw au Suufiyyah katika mfumo sahihi. Kwa nini? Kwa kuwa asiyekuwa na kitu hawezi pia kutoa kitu. Kazi yao hivi sasa ni kuwaharibu watu wema ambao Allaah Amewaongoza katika mfumo Wake. Kazi yao leo ulimwenguni mzima ni kuwawinda vijana Salafiyyuun. Wakati wa kuwawinda wanavaa mavazi ya Salafiyyah ili waweze kuwatoa katika mfumo huu. Wanatumia mifumo mbalimbali ili kuchafua mfumo huu wa wanachuoni – na tunaomba kinga kwa Allaah.

Zaidi ya hayo, wanaupa kipaumbele mfumo wa Sayyid Qutwub hata kama utakuwa na kuwatukana Manabii, Takfiyr kwa baadhi ya Maswahabah, Takfiyr kwa Ummah na kadhalika. Pamoja na kuwa ana madhehebu potevu kama ya Huluuliyyah, Wahdat-ul-Wujuud, kukanusha Sifa za Allaah, kauli ya kusema kwamba Qur-aan imeumbwa na mengi, hayaendi kinyume na mageuzi machoni mwao. Bado ni Mujaddid, kwa mujibu wao!

Sisi tunasema “ndio” ni Mujaddid. Ni Mujaddid wa Bid´ah zote kubwa: madhehebu ya Khawaarij, Rawaafidhw, Murji-ah, Jabriyyah, Suufiyyah, falsafa za kimashariki na za kimagharibi. Amejadidi yote hayo. Baina yetu na sisi tuna vitabu vya Sayyid Qutwub na kazi zake.

Huyu bado wanamchukulia kuwa ni Mujaddid na Imaam. Wanajenga mapenzi na chuki kwa ajili yake. Kuna balaa ipi kubwa juu ya Uislamu kushinda balaa hii?!

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26874
  • Imechapishwa: 19/05/2015