Ndio maana Qur-aan inatakiwa kusomwa kwa sauti nzuri

Swali: Baadhi ya ndugu wametangulia kuuliza kuhusu Hadiyth:

”Ipambeni Qur-aan kwa sauti zenu.”

Jibu: Hadiyth iliyotajwa baada ya kuihakiki imethibiti kuwa ni Swahiyh. Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud, an-Nasaa´iy, Ibn Maajah na ad-Daarimiy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kutoka kwa al-Baraa´ bin ´Aazib (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ipambeni Qur-aan kwa sauti zenu.”

Kwa hiyo kuipamba Qur-aan kwa sauti ni miongoni mwa sababu za unyenyekevu na mazingatio. Vilevile ni miongoni mwa sababu za kuwa na shauku kusikiliza Qur-aan na pia ni miongoni mwa sababu za kutaka kufahamu kile anachosema Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21706/ما-صحة-حديث-زينوا-القران-باصواتكم
  • Imechapishwa: 24/09/2022