Pili: Kukubali kwa al-Khaliyliy ya kwamba Allaah anasifika kwa sifa ya maneno kwa kuwa ni sifa kamilifu na akashikamana na hilo, haya ndio yanayolinganiwa na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na kuyaamini na vilevile ndio aliyoyathibitisha Allaah katika Kitabu Chake. Hakika Allaah amewaibisha wana wa israa´iyl pindi walipojichukulia mungu badala ya Allaah kwa vile aliwabainishia kuwa moja katika mapungufu yake ni kwamba hazungumzi na wala hawaongoi njia. Amesema (Ta´ala):

وَاتَّخَذَ قَوْمُ مُوسَىٰ مِن بَعْدِهِ مِنْ حُلِيِّهِمْ عِجْلًا جَسَدًا لَّهُ خُوَارٌ ۚ أَلَمْ يَرَوْا أَنَّهُ لَا يُكَلِّمُهُمْ وَلَا يَهْدِيهِمْ سَبِيلًا ۘ اتَّخَذُوهُ وَكَانُوا ظَالِمِينَ

“Watu wa Muusa walijifanyia, baada ya kuondoka kwake katika mapambo yao, umbo la ndama. Je, hawakuona kuwa huyo [ndama] hawasemeshi na wala hawaongozi njia? Walimfanya [kuwa mungu] na wakawa madhalimu.”[1]

Allaah amemuabisha mungu huyu aliyefanywa kuwa mungu badala Yake na kubainisha kuwa moja katika mapungufu yake ni kuwa hazungumzi. Amesema (Ta´ala) katika Aayah nyingine:

أَفَلَا يَرَوْنَ أَلَّا يَرْجِعُ إِلَيْهِمْ قَوْلًا

“Je, hawaoni kuwa [huyo ndama] hawarudishii neno.”[2]

Ikapata kutambulika kushindwa kuzungumza na kutoa neno ni upungufu unaotumiwa kama hoja ya ndama kutostahiki kuwa mungu.

[1] 07:148

[2] 20:89

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 161
  • Imechapishwa: 14/01/2017