Ndio maana mashaytwaan wa kibinaadamu ni khatari zaidi

Swali: Ni kwa nini mashytwaan wa kibinaadamu ni khatari zaidi kuliko mashaytwaan wa kijini?

Jibu: Kwa sababu mashaytwaan wa kibinadaamu wanadai kuwa ni ndugu zako na majina yao vilevile huwa ni mazuri kama “Muhammad”, “´Aliy”, “Swaalih”. Isitoshe wanakaa pamoja na wewe, wanakutapa na wewe unawaamini. Hili ni tofauti na mashaytwaan wa kijini ambao huwaoni. Mashaytwaan wa kijini huwaoni tofauti na mashaytwaan wa kibinaadamu ambao unawaona, wanakuja kukaa pamoja na wewe, wanaingia nyumbani kwako na wanaapa kuwa ni wenye kukutakia kheri na madai mengine tele. Hawa wana khatari zaidi kuliko mashaytwaan wa kijini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (02) http://alfawzan.af.org.sa/node/2045
  • Imechapishwa: 11/10/2016