Allaah (Ta´ala) amesema:

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Basi naapa kwa Mola wako hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana kati yao, kisha wasipate katika nyoyo zao kigegezi katika yale uliyohukumu na wajisalimishe kabisa.” (04:65)

Allaah amekataa kuwa yule asiyehukumiwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hana imani. Je, Ahl-ul-Ahwaa´ wamehukumiana na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika yale yanayokwenda kinyume na Qur-aan na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Ninaapa kwa Allaah lau wangefanya hivi basi kusingelipatikana tofauti hizi.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=7539
  • Imechapishwa: 06/09/2020