Ndio maana ikafaa kumswalia maiti makaburini

Swali: Je, mtu anaweza kutumia Hadiyth ya yule mwanamke mweusi kwamba inafaa kuswali makaburini?

Jibu: Ni sawa na haina neno kumswalia maiti makaburini. Ambacho hakijuzu ni swalah isiyokuwa na Rukuu´ na Sujuud. Ama kuhusu kumswalia maiti makaburini haina neno. Ni kitu kilichofanywa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Inaitwa swalah ya jeneza ambayo ni du´aa. Malengo yake ni du´aa. Akiiswali makaburini haina neno. Imefanywa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Swali: Hata kama kumeshapita muda mrefu?

Jibu: Iwe mwezi mmoja na chini ya hapo. Ikiwa hajapitikiwa na mwezi mmoja au mfano wake basi aswalie kaburi lake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21612/حكم-الصلاة-على-الميت-في-المقبرة
  • Imechapishwa: 28/08/2022