Wakati wanapotuponda hawafanyi hivo kwa sababu ya jambo lenyewe. Wanatuponda kwa sababu wametuomba tokea zamani. Wametuomba tusiwazungumzie, hatukukubali hilo. Hatutonyamaza kabisa:

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Na uweko kutoka kwenu Ummah unaolingania kheri na unaoamrisha mema na unaokataza  maovu na hao ndio waliofaulu.” (03:104)

Ni lazima lipatikane hili. Ni lazima kupatikana ulinganio katika Dini ya Allaah, kuamrisha mema na kukataza maovu. Hatutonyamazia upotevu huu. Mnamsifu ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq. Mnamsifu ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy. Si wewe ndiye ulisema, Muhammad al-Mahdiy, ya kwamba ni wajibu kwa ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy kumcha Allaah kwa vijana wanaomfuata na kuwanasihi kuwa na utulivu na kusoma na asiwapoteze? Ulikuwa na ujuzi kuhusu kosa la al-Ikhwaan al-Muslimuun. Nilikuwa nikisema kuwa huna mfano inapokuja katika ujuzi wa upotevu ulioko kwa al-Ikhwaan al-Muslimuun. Lakini hivi sasa umekuwa mpumbavu. Lau ungelisema haki. Umekuwa mpumbavu na umekuwa sasa ni mwenye kuwavamia Ahl-us-Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=20
  • Imechapishwa: 14/07/2020