Je, kumthibitishia Allaah usikizi kunapelekea kumthibitishia vilevile masikio? Hakupelekei. Je, kumthibitishia Allaah uoni kunapelekea kumthibitishia vilevile macho? Hakupelekei. Kujengea juu ya haya tunasema kuwa hatumthibitishii Allaah masikio. Haikupokelewa kwamba Allaah anayo masikio. Lakini tunamthibitishia Allaah macho mawili, sio kwa sababu ya Aayah hii bali ni kutokana na Aayah nyenginezo. Kwa mfano maneno Yake (Ta´ala):

وَلِتُصْنَعَ عَلَىٰ عَيْنِي

”…  ili ulelewe Machoni Mwangu.” (20:39)

تَجْرِي بِأَعْيُنِنَا

”… inatembea kwa macho Yetu.” (54:13-14)

Pengine mtu akauliza: ni kwa nini kuthibitisha usikizi hakupelekei vilevile kuthibitisha masikio? Hatufanyi hivo. Je, ardhi siku ya Qiyaamah si itaelezea khabari zake[1] na zile kheri na shari, maneno na matendo yaliyofanywa juu yake? Je, ardhi inayo masikio? Hapana.

[1]  99:4

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=vRU4IY8_bO0
  • Imechapishwa: 11/10/2020