Ndio maana bima zote ni haramu

Swali: Yule mwenye kuzisifu bima za biashara na kusema kwamba zina faida na kwamba zina manufaa katika jamii pamoja na kwamba hazifai – je, anazingatiwa ametoka nje ya Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Bima, kwa aina zake zote kukiwemo za biashara, ni haramu. Kwa sababu ni kula mali za watu kwa batili. Ndani yake kuna ribaa, madhara, hali ya kutokujua, kamari n.k. Bima ina maafa mengi. Yule mwenye kusema kwamba bima ina manufaa, ni kama tulivyokutajieni hapo kabla. Kule kupatikana manufaa katika kitu haifahamishi juu ya uhalali wake mpaka mtu alinganishe yale manufaa yaliyomo na madhara. Ikiwa madahara ya kitu hicho ndio mengi zaidi au yanalingana, basi ni haramu. Bima madhara yake ni mengi zaidi. Ndani yake kuna dhuluma, kula mali za watu kwa batili, ribaa, kamari, kuziweka pesa khatarini n.k. Kwa mfano wewe unatoa Riyaal 100 na unapofikwa na ajali unapokea milioni moja. Ni kwa kitu gani kimekufanya wewe ustahiki kula milioni hii? Ni kutoka katika mali za watu. Kampuni haitoi kitu. Hizi ulizopokea ni pesa za watu zilizokusanywa. Umekula pesa za watu kwa batili. Wewe hukutoa isipokuwa tu Riyaal 100. Yote haya ni batili. Madhara yake ni makubwa kuliko manufaa yake.

Wako ambao wamejuzisha bima kutokana na Ijtihaad zao japo wamekosea. Kunasemwa kwamba wametoka nje ya mipaka ya kuhalalisha kilicho haramu. Wamehalalisha kitu kilicho cha haramu pasi na kukusudia. Amedhania kuwa ni sawa na sahihi pamoja na kwamba amekosea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (09) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/09.mp3
  • Imechapishwa: 06/04/2019