Ndio maana bado watu wanaendelea kufanya maasi


Swali: Vipi tunaona shari na maasi mengi katika Ramadhaan ilihali tunaambiwa kuwa mashaytwaan wamefungwa?

Jibu: Watu wako aina mbili:

1- Makafiri. Hawa hawana ulinzi wa shaytwaan na khaswa wale wanaojua kuwa wataingia Motoni milele na hawatotoka ndani yake.

2- Waumini. Muumini hupunguza kufanya maasi. Makusudio si kwamba ni viumbe wote.

Kama tulivotangulia kusema watu wako aina mbili; makafiri ambao hubaki katika ukafiri na upotevu wao na waumini ambao hupunguza kufanya maasi. Haya ndio malengo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=RngN2JIBtjs
  • Imechapishwa: 19/05/2020