al-Halabiy amesema:

“Ninakariri ya kwamba haina maana kuwa nachukulia sahali katika haki kwenye masuala waliyokosolewa. Tuliwabainisha kabisa, tukawaraddi na kuwabatilisha. Pamoja na hivyo yote haya yanafanywa kwa ajili ya manufaa yao wenyewe na kwa kuwajali warejee katika haki ambayo wanakwenda kinyume nayo na wanachuoni wetu.”

Yote haya tunayafanya kwa ajili ya manufaa yao wenyewe na kwa kuwajali wao na wengine wenye kudanganyika na maneno yao. Walipoyashikilia makosa yao Ahl-us-Sunnah wakawanasihi kwa siri na hadharani. Wakiendelea kuyashikilia madhambi yao na kukataa kupokea nasaha, ni wajibu kwa Ahl-us-Sunnah kubainisha batili yao na kuwafichua ili asiwepo yeyote atayedanganyika nao. Haijuzu kwa yeyote katika Ahl-us-Sunnah kunyamazia batili yao kwa sababu ya upendeleo, kupakana mafuta au kitu kingine.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Durar an-Najmiyyah fiy Radd-ish-Shubuhaat al-´Aqadiyyah wal-Manhajiyyah, uk. 391-392
  • Imechapishwa: 18/03/2017