Swali: Istihzai imegawanyika mafungu mangapi? Kuna kidhibiti katika kuwafanyia istihzai wanachuoni?

Jibu: Mara nyingi na dhahiri kwa yule mwenye kuwafanyia mzaha wanachuoni anakuwa anafanya hivo kutokana na ile elimu waliyobeba na si kwamba anafanya hivo kwa sababu ya wao kama wao. Hawasemi kwamba fulani ni kiguru, chongo au kitu fulani mwilini mwake. Haifai kumfanyia hivi muislamu. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَىٰ أَن يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِّن نِّسَاءٍ عَسَىٰ أَن يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ

“Enyi walioamini! Wanaume wasiwadharau wanaume wengineo huenda wakawa bora kuliko wao wala wanawake kwa wanawake wengineo.” (49:11)

Hakuwafanyia istihzai wanachuoni isipokuwa kwa sababu ya ile elimu yao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (06)
  • Imechapishwa: 30/12/2018