Ndio maana Ahl-ul-Bid´ah wanapinga Hadiyth ya kugawanyika kwa Ummah


Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mayahudi wamegawanyika katika makundi sabini na moja. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja. Manaswara wamegawanyika katika makundi sabini na mbili. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja. Na Ummah huu utakuja kugawanyika katika makundi sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja.” Akaulizwa: “Ni kina nani hao, ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni wale wenye kufuata yale niliyomo mimi hii leo na Maswahabah zangu.”

Kuhusiana na wale wenye kuamini Hadiyth hii – na ni Hadiyth Swahiyh – wanaitendea kazi na kuwatahadharisha waislamu na maangamivu na kuwaelekeza katika yale aliyokuwa akifuata Mtume na Maswahabah zake.

Ama kuhusiana na Ahl-ul-Ahwaa´ wanapindisha maana sahihi ya Hadiyth hii na wakati mwingine wanadai kuwa ni dhaifu[1]. Ni kwa nini wanafanya hivo? Ni kwa sababu Hadiyth hii inabainisha upotevu waliyomo na inawashuhudilia maangamivu. Wanapata maslahi kwa mfarakano huu. Watu hawa wana wafuasi wenye kuwatumia na kuheshimu hadhi zao. Ili kuhifadhi hadhi hizi na mslahi yao ya kidunia, ndio maana wanapinga Hadiyth hii ili heshimao yao ibaki au angalau kwa uchache wanaipindisha maana yake sahihi. Wanapindisha maana yake sahihi ili waweze kubaki katika upindaji waliyomo na ili Hadiyth hii isije ikawafichue na kuwafedhehesha. Hatimaye vijana waje kuwaambia “Mbona hamfuati pote lililookoka? Ni kwa nini mnabaki katika upotevu huu? Ni kwa nini mko katika mapote haya yaliyoangamia?” Kwa ajili hiyo ndio maana wanawapaka mchanga wa machoni.

[1] Tazama http://firqatunnajia.com/ni-hadiyth-swahiyh/

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=7539
  • Imechapishwa: 06/09/2020