Nchi zinazolazimisha kuweka bima katika gari

Nasaha zangu kwa ndugu zangu wote waislamu wamche Allaah (´Azza wa Jall) na wasifanye maharamisho ya Allaah. Watambue kuwa mali imeumbwa kwa ajili yao na si kwamba wameumbwa kwa ajili ya mali. Watambue vilevile kwamba mali ima ikamtoka mtu katika maisha yake au mtu akafa na ikarithiwa na wale warithi wake. Kwa hivyo bima kwa aina zake zote ni haramu.

Lakini tumeambiwa kwamba baadhi ya miji inawalazimisha watu kuweka bima na hawampi mtu rukhusa ya kuendesha gari wala mu´amala mwingine wowote isipokuwa mpaka mtu aweke bima. Katika hali hii mtu afanye nini? Tunasema kuwa hii ni dharurah. Wape kile walichokuomba katika hiyo bima. Lakini utapopatwa na kitu usichukue kutoka kwao isipokuwa kwa kiwango kilekile ulichowapa. Kwa sababu mkataba ulio kati yenu ni batili kwa mujibu wa Shari´ah. Ikiwa umeshakuwa batili basi kinabatilika vilevile kile kinachopelekea katika mkataba huu na hivyo si halali kwako kupokea isipokuwa kiwango kilekile ulichowapa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (59) http://binothaimeen.net/content/1348
  • Imechapishwa: 21/11/2019