Nchi ya Kiislamu ambayo mtu hawezi kutekeleza dini

Swali: Kusafiri kwenda katika miji ya kiislamu ambayo hukumu zake ni za kikafiri kunazingatiwa ni kusafiri kwenda katika miji ya kushirikina khaswa ukizingatia kwamba kuna dini zengine huko kama mfano wa unaswara, Nusayriyyah na nyenginezo?

Jibu: Ikiwa hawezi kudhihirisha dini yake[1] haitofaa kwake kusafiri. Ikiwa anaweza kudhihirisha dini yake, anaweza kujibu mambo ya utata na kubainisha vilevile mambo mazuri ya Uislamu, wakati wa kuhitajia kufanya hivo hapana ubaya. Haijuzu kwake kusafiri kwenda katika nchi yoyote ile ambayo hawezi kutekeleza dini yake.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/maana-ya-kudhihirisha-dini-katika-miji-ya-kikafiri__trashed/

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (09) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191370#219699
  • Imechapishwa: 06/03/2019