Swali: Muulizaji kutoka Misr anauliza, je kutoka katika mamlaka ya mtawala ni haramu kwa dhati yake au kwa sababu ya madhara makubwa yanayopatikana?

Jibu: Ni Haramu kwa dhati yake na madhara. Huwezi kukuta kitu ambacho kaharamisha Allaah na Mtume Wake isipokuwa uharamu huo unarudi kwa maslahi ya mtu mwenyewe. Atakayesalimika kutokana na harakati hizi za maandamano yaliyopitika na hayakufikia mauaji Tunisia na Misr… Isitoshe kipi kinachoendelea Misr tangu maandamano yaanze mpaka hivi leo?

Watu wengi wajinga wameenda kuwasababishia madhara wengine. Wameenda kuvamia na kutaka kubadili serikali na mambo mengine mengi. Jambo hili ni kubwa sana!

Kama ninavyosema zaidi ya mara moja, maandamano ya kwanza yaliyopatikana katika Uislamu ilikuwa wakati wa ukhalifah wa kiongozi mwema ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh) na Radhi za Allaah ziwaendee Maswahabah wa Mtume Muhammad wote. Hii ndio ilikuwa sababu ya kuuawa ´Uthmaan bin ´Affaaan (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.youtube.com/watch?v=23IZyoqBEBg
  • Imechapishwa: 06/09/2020