Swali: Kuna ndugu anauliza hukumu ya kuoa mnaswara mwema. Amemuahidi kuingia katika Uislamu baada ya kumfunza. Lakini anaogopa asije kukosa kuingia.

Jibu: Anaweza kumuoa hata kama atabaki kwenye unaswara wake. Allaah (´Azza wa Jall) amehalalisha hilo:

وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ

“… na [pia mmehalalishiwa kuwaoa] wanawake wenye kujichunga na machafu miongoni mwa Ahl-ul-Kitaab kabla yenu.” (05:03)

bi maana ni halali.

Anachotakiwa tu ni kujitahidi kufanya sababu za kumwingiza katika Uislamu. Mwanamke anaweza kuwa na shauku na kutamani, atakuwa – Allaah akitaka – ni mwenye kuharakia kukubali. Akimbainishia uzuri wa Uislamu na akamkirimu, ataingia katika Uislamu. Kwa kule mwanaume kuwa na taathira kwa mwanamke ikawa inajuzu kwake kumuoa myahudi na mnaswara na yeye ni muislamu. Lakini yeye mwanamke hana taathira kwa mume. Haijuzu kwake mwanamke kuolewa na mwanaume myahudi au mnaswara au kafiri. Haijuzu kamwe kwa kutokuwa na uwezo wa kumuathiri. Ama mwanaume ana taathira. Kama alivyosema Allaah (´Azza wa Jall):

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ

“Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake.” (04:34)

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.njza.net/Default_ar.aspx?ID=98
  • Imechapishwa: 22/09/2020