Nasaha za Ibn Baaz kwa wanawake wote

Swali: Tunatumai kutoka kwako muheshimiwa kuwapa nasaha wanawake khaswa kwa kuzingatia kwamba wapo hapa na Allaah akujaze kheri.

Jibu: Nawausia dada zangu wote kwa ajili ya Allaah wamche Allaah. Vilevile nawausia kumtii Allaah, kuwa na msimamo katika dini, kuhifadhi swalah kwa mkusanyiko ndani ya wakati wake, kumsikiliza na kumtii mume katika ambayo ni mema, kutahadhari kutokamana na kuonyesha mapambo, kuonyesha uso na sababu za fitina. Nawausia dada wote kumcha Allaah, wahifadhi swalah ndani ya wakati wake nyumbani pamoja na utulivu na unyenyekevu na kutahadhari kutokamana na kuonyesha mapambo, jambo ambalo linawadhuru waislamu wa kiume na kutahadhari kutokamana na maasi yote kama mfano wa usengenyi, umbea, kumuasi mume bila ya haki na mfano wa hayo. Kwa hiyo tunawausia wote kumcha Allaah, kusaidiana juu ya wema na kumcha Allaah na kuishi kwa wema. Vivyo hivyo tunawausia waume hayo. Tunawausia wote kumcha Allaah na kusaidiana juu ya wema na kumcha Allaah. Amesema (Ta´ala) amesema:

وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ

“Kaeni nao kwa wema.”[1]

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ

“Na shirikianeni katika wema na taqwa.”[2]

Tunawausia wote kumcha Allaah, kusaidiana juu ya kheri na kutahadhari kutokamana na yale yote aliyokataza Allaah na Mtume Wake.

[1] 04:19

[2] 05:02

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3755/%D9%86%D8%B5%D9%8A%D8%AD%D8%A9-%D8%AC%D8%A7%D9%85%D8%B9%D8%A9-%D9%84%D9%84%D9%86%D8%B3%D8%A7%D8%A1-%D9%85%D9%86-%D8%A7%D9%84%D8%B4%D9%8A%D8%AE-%D8%A7%D8%A8%D9%86-%D8%A8%D8%A7%D8%B2
  • Imechapishwa: 06/03/2020