Nasaha za al-Waadi´iy kwa mume na mke ambao ni wanafunzi

Swali: Ni katika mpaka upi ambao ni wajibu kwa mwanamke kumtii mume wake?

Jibu: Ama masuala ya wajibu, anatakiwa kumtii katika yale mambo ambayo Allaah Kamuwajibishia juu yake. Miongoni mwayo, ni pale ambapo atamwita kitandani. Na ikiwa mume ni fakiri, inatakikana kwa mwanamke awe na subira kwake kadiri na atakavyoweza.

Pamoja na hivyo, kuna jambo ambalo ni pana zaidi kuliko uwajibu huu. Na jambo hilo sisi tunamnasihi amvumilie mume wake katika raha na shida, asimkalifishe mume kwa asiyoyaweza na kununua mambo mapya. Akiona gari na nguo mpya, anamuomba mume wake amnunulie mfano wa gari hii na nguo hiyo. Inatakikana kwake awe na subira na mume wake, amtendee wema, kuwalea watoto wake, amfulie nguo zake, amsaidie katika kheri na amtengenezee chakula kizuri pale itapohitajika kufanya hivyo. Wawe ni wenye kusaidizana na khaswa pale ambapo nyinyi nyote ni wanafunzi wanaume na wanawake. Muda unaweza kuwa mfinyu kwa mwanamke na hilo likasababisha akawa na mapungufu katika baadhi ya haki za mume wake. Katika hali hii, inatakikana mume kuwa na subira kwa mke wake. Na muda unaweza kuwa mfinyu kwa mume na akawa na mapungufu katika baadhi ya haki za mke wake. Katika hali hii, inatakikana mke kuwa na subira kwa mume wake.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1733
  • Imechapishwa: 17/02/2018