Nasaha Shaykh al-Fawzaan kwa wanawake jinsi ya kuhifadhi dini yao


Swali: Tunaomba utupe nasaha sisi kundi la wanawake vipi tutaihifadhi dini yetu, wasichana wetu, wavulana wetu na waume zetu?

Jibu: Mtawahifadhi kwa…

1- Kumuomba Allaah (´Azza wa Jall) msaada.

2- Kuamrisha mema na kukataza maovu.

3- Kuwalea wavulana na wasichana katika kumtii Allaah. Kama alivyosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Waamrisheni watoto wenu swalah kwa miaka saba. Wapigeni kwa ajili yake [hiyo swalah] katika umri wa miaka kumi na watenganisheni katika vitanda.”

4- Waleeni katika kumtii Allaah na katika dini na katika tabia nzuri.

5- Waepusheni mbali na tabia mbaya. Watenganishwe kwenye vitanda. Kwa ajili ya nini? Ni kwa ajili ya kulinda utwaharifu wao kutokana na fitina. Katika hili kuna dalili ya kukatazwa mchanganyiko baina ya wanaume na wanawake. Hata watoto wadogo ambao wamekaribia kubaleghe hawaachwi wakachanganyika kwenye kitanda kimoja. Watenganishe na wala wasiachwe wakalala mahala pamoja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13517
  • Imechapishwa: 20/09/2020