Nasaha kwa wazazi wenye kupoteza wakati wao mbele ya TV

Swali: Natarajia utawapa nasaha mababa na mababu ambao miaka yao imepita sitini na nywele za kichwani mwazo na ndevu zao zimeshapita mvi na miili yao imeshakuwa dhaifu. Lakini pamoja na haya yote usiku mzima wanaishi mbele ya vipindi vya TV na filamu na hawakubali badala ya hayo chochote kabisa. Bali wakati mwingine swalah ya Fajr na ´Aswr zinawapita na hawahifadhi Witr wala swalah za sunnah. Hawajali nyimbo zinazochezwa humo wala majanga yanayoonekana humo. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba nyoyo za watoto zinaingia khasarani na huku wao hawajali.

Jibu: Nawaambia watu hawa wamche Allaah juu ya nafsi zao. Ni wajibu kwa mzazi awe kiigizo chema kwa familia yake na kizazi chake na asiwe ni kiigizo kiovu. Watahadhari kule shaytwaan kucheza na wao na kupoteza wakati wao katika yale ambayo hayamridhishi Allaah (´Azza wa Jall). Watambue kuwa watoto wao watakapowaona katika hali hii watawaiga. Nasaha zangu kwao:

Mosi: Wasishiriki katika yale yaliyotajwa na muulizaji.

Pili: Wafanye bidii katika kuwapa watoto wao malezi yaliyo mazuri na wakubali nasaha kutoka kwa watoto wao na khaswa pale ambapo watoto wao watakuwa ni wema ambao Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewatunuku elimu na matendo.

Tunamuomba Allaah sisi na wao awape usalama na afya.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (31) http://binothaimeen.net/content/711
  • Imechapishwa: 05/11/2017