Nasaha kwa watu wa Libya

Waislamu ni wenye wasiwasi juu ya fitina ya leo inayoendelea Libya na nyinginezo katika nchi za waislamu zilizosibiwa na fitina hii leo. Ni wajibu kwa watu wa Libya kushirikiana ili kusimamisha fitina hii, kila mmoja kwa kiasi na uwezo wake. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ

“Shirikianeni katika wema na uchaji Allaah na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. Na Mcheni Allaah; hakika Allaah ni mkali wa kuadhibu.” (05:02)

Watu wote wa Libya ni lazima kujiunga katika uongozi wa Shari´ah na wahukumiwe nayo. Haki ni moja na sio nyingi. Ikiwa watu wanataka haki basi watakuwa na umoja, na matamanio yakitofautiana watagawanyika. Allaah Ameamrisha umoja na mkusanyiko na Akakataza kufarakana na kutofautiana. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا

“Shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja wala msifarikiane.” (03:103)

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

“Na wala msiwe kama wale ambao walifarikiana na wakakhitilafiana baada ya kuwajia hoja za wazi. Na hao watapata adhabu kuu.” (03:105)

وَلَا تَنَازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ

”Na wala msizozane, mtavunjikwa moyo, na itapotea nguvu yenu, na subirini. Hakika Allaah Yu Pamoja na wanaosubiri.” (08:46)

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ

“Hakika waumini ni ndugu, basi suluhisheni baina ya ndugu zenu. Na Mcheni Allaah ili mpate kurehemewa.” (49:10)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mfano wa waislamu katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao na kuhisiana kwao ni kama mfano wa mwili mmoja. Kiungo kimoja kikipata maumivu, mwili mzima unapata maumivu kwa homa na kutopata usingizi.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Abu Muusa (Radhiya Allaahu ´anh).

Katika kila njia kunafikiwa manufaa na kuzuiwa madhara kupitia mtawala wake. Akitiiwa katika yanayojuzu kunafikiwa amani. Maisha ya kidini na dunia yanakuwa katika hali nzuri. Hakuna nchi inayoweza kuwa na umoja isipokuwa kwa uongozi na uongozi hauwezi kufikiwa isipokuwa kwa utiifu. Vinginevyo kunakuwa dhuluma na machafuko pindi Ahkaam za Kishari´ah, Swalah za Ijumaa na Swalah za Jamaa´ah vinapoondolewa. Inasababisha watu kuwa katika khofu na maisha magumu. Hali mbaya inakuwa tu mbaya zaidi.

Watu wa Libya ni wajibu kwao kujiunga na mtu aliye na utawala Libya na wale wanaopambana na kusaidizana kupatikana serikali ya kudumu. Serikali hii yenye kudumu ambayo wanapambana iweze kupatikana inatakiwa iwe kwa mujibu wa Shari´ah, mashauriano na maafikiano ya Ahl-ul-Hall wal-´Aqd ambao wanajulikana kutaka Uislamu na manufaa ya Libya. Mashauriano yanatakiwa yapitike kwa jeshi la ki-Libya kuchunga nidhamu ya mambo, wanachuoni wa Libya wenye kujulikana kwa elimu, msimamo na kushikamana na mfumo wa Maswahabah na waliokuja baada yao na kwa watu wenye akili walio na busara njema na viongozi wa makabila wanaojulikana. Watapokubaliana juu ya manufaa ya Uislamu, waislamu na nchi yao, ni wajibu kuwasapoti katika hayo.

Yule mwenye kwenda kinyume na haki ambayo watakuwa wameafikiana nayo na kwa umoja wa rai wa Libya, basi azuiwe kwa njia khafifu iwezekanayo kusitisha shari yake. Atahadharishwe naye hata kama atajiita kwa majina ya Kiislamu kama mfano wa kundi linalojiita “Answaar-us-Shari´ah”. Kinachozingatiwa ni uhakika wa mambo. Lengo ni kuingiza haki na kuangusha batili. Vijana wengi wanapelekwa na hisia za Kiislamu na maneno ya kuvutia pasina elimu juu ya mapote mbali mbali yanayowaelekea. Kwa sababu ya ujinga wao wanatumbukia ndani ya kitu kisichokubaliwa na Uislamu.

Kadhalika walibya wote na watu waliosafiri huko ni wajibu kutomwaga damu. Allaah Ameziharamisha damu za waislamu, mali zao na heshima yao, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Khutbah yake ya Hajj ya kuaga.

Vilevile ni lazima kujitenga mbali na mambo ya ulipuaji, mauaji, utekaji nyara na Takfiyr kwa waislamu. Mambo yote haya ni madhambi makubwa ambayo madhara yake yanajuwa Allaah pekee. Ni usaliti na khiyana. Yanasababisha jamii ya Kiislamu kuwa dhaifu.

  • Mhusika: Shaykh ´Aliy bin ´Abdir-Rahmaan al-Hudhayfiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=144291
  • Imechapishwa: 23/04/2015