Nasaha kwa watazamaji wa TV


Swali: Ni ipi hukumu ya kutazama TV?

Jibu: Kutazama TV ni khatari sana. Mimi nashauri kutoitazama na kutokaa mbele yake kiasi na vile mtu atavyoweza. Lakini ikiwa yule mtazamaji ana [imani yenye] nguvu ambapo anaweza kufaidika nayo katika mambo yenye kheri na haiwezi kumpelekea katika shari, basi hapo hakuna neno. Hapa ni pale atapokuwa na [imani yenye] nguvu anayoijua moyoni mwake ambapo anaweza kusikiliza kitu kizuri na akafaidika nacho na akajiepusha na kitu kibaya kama vile nyimbo, maigizo mabaya na mengineyo yanayoidhuru jamii. Katika hali hii hakuna neno. Lakini mara nyingi baadhi ya mambo yanayavuta mengine. Kwa ajili hiyo mimi nashauri kutoiingiza nyumbani na kutoitazama. Kwa sababu baadhi ya mambo huvuta mengine. Sababu nyingine ni kwa kuwa nafsi ni yenye kuvutikiwa kutazama mambo ya kigeni mbele yake. TV sio kama kifaa cha kusikiliza tu. Kifaa cha kusikiliza khatari yake ni afueni. Mwenye kutazama na huku anasikiliza nafsi yake inakuwa ni yenye kumili zaidi na kufungamana kwake na kitu hicho kunakuwa kukubwa zaidi.

Baya na chafu zaidi kuliko haya ni video pindi mtu atakuwa amerekodi ndani yake filamu chafu zinazoenezwa na watu. Filamu hizi chafu zinazokuwa kwenye video shari yake ni kubwa zaidi. Ni wajibu kutahadhari na hilo. Ni wajibu kwa mwenye akili akiona kitu katika hayo basi aichane ile kanda au badala yake arekodi kitu kingine ambacho kinafuta video hii chafu ikiwa anaweza kufanya hivo. Badala yake arekodi kitu kingine chenye manufaa ambacho kitafuta ule uchafu uliomo ndani na afaidike na kanda yake ambayo amerekodi kitu chenye manufaa.

Baya zaidi kuliko hiyo ni dishi. Ni wajibu kutahadhari nayo na kutoiingiza katika majumba. Allaah awalinde waislamu kutokamana na shari ya vyote hivi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3231/%D9%86%D8%B5%D9%8A%D8%AD%D8%A9-%D9%84%D9%85%D9%86-%D9%8A%D8%B4%D8%A7%D9%87%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D9%84%D9%81%D8%A7%D8%B2
  • Imechapishwa: 07/10/2018