Nasaha kwa wasimamizi wa masomo wasiowaacha wanafunzi kuswali kwa wakati

Swali: Kuna baadhi ya watu wanachelewesha wakati wa swalah kwa wakati wake kwa hoja ya kwamba wanakuwa kazini au wanakuwa na muhadhara. Mwanafunzi akichelewa wakati huu basi anaweza kuzuiwa kuingia kazini au kwenye muhadhara. Wafanye nini na khaswa kwa kuzingatia ya kwamba baadhi ya wanafunzi shuleni hawaswali?

Jibu: Ninachowanasihi wasimamizi wamche Allaah juu ya Ummah huu na wajali hisia za waislamu. Ni nini demokrasia? Ni mambo ya uongo. Demokrasia ya kikafiri na sio ya waislamu. Vinginevyo wewe ni muislamu. Unachotakiwa ni kwenda kuswali na kumuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kisha urudi katika kazi yako. Haijuzu kuchelewesha swalah kwa ajili ya kazi kama hii. Hakika kitendo cha kuchelewesha swalah… labda ikiwa ni kuchelewesha mpaka mwisho wa wakati wake. Kuhusu kuacha swalah ya mkusanyiko na waislamu wenzako, hakika tambua kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitaka kuunguza majumba ya wale wanaume wenye kuacha kuja kuswali pamoja na waislamu wenzo. Kilichomzuia ilikuwa ni wanawake na watoto. Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna kati ya mja na kufuru au shirki isipokuwa swalah.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumpa idhini Ibn Umm-Maktuum – kama ilivyokuja katika “as-Swahiyh” ya Muslim – ya kuacha swalah ya mkusanyiko. Swalah ya mkusanyiko inazingatiwa kuwa ni wajibu.

Mimi nasema muislamu anatakiwa ajifakhari kwa dini yake:

وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِّمَّن دَعَا إِلَى اللَّـهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ

“Ni nani mwenye kauli nzuri zaidi kuliko yule anayelingania kwa Allaah na akatenda mema na akasema: “Hakika mimi ni miongoni mwa waislamu.” (41:33)

Wewe unauza dini yako kwa sababu ya vyeti? Allaah atakupa kilicho bora badala yake:

“Yule mwenye kuacha kitu kwa ajili ya Allaah, basi Allaah atampa bora kuliko hicho.”

Wasimamizi hawa wanatakiwa kunasihiwa. Wakikubali ni jambo zuri. Wasipokubali basi mimi nakunasihini muache masomo hayo. Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hatokutupeni.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=103
  • Imechapishwa: 15/03/2018