Nasaha kwa wapenzi wa picha


Swali: Una nasaha yoyote kuwapa wale ambao wamekithirisha kupiga picha kwenye msiktii mtakatifu wa Makkah na imekuwa ni kama vile ni sehemu ya utalii?

Jibu: Picha ni haramu sawa kwenye msikiti wa Makkah na kwenginepo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani watengeneza picha. Amesema kuwa wao ndio watu wataokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah. Wao ndio madhalimu wakubwa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth ya kiungu ya kwamba Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

“Ni nani dhalimu mkubwa ambaye anaumba kama viumbe Wake.”

Bi maana watengeneza picha.

Picha ni haramu. Imeharamishwa vibaya sana. Ni dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa. Zikipigwa kwenye msikiti mtakatifu wa Makkah khatari inaongezeka:

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ الَّذِي جَعَلْنَاهُ لِلنَّاسِ سَوَاءً الْعَاكِفُ فِيهِ وَالْبَادِ ۚ وَمَن يُرِدْ فِيهِ بِإِلْحَادٍ بِظُلْمٍ نُّذِقْهُ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ

“Hakika wale waliokufuru na wanazuia watu njia ya Allaah na [pia wanazuia watu wasifike] al-Masjid al-Haram ambao Tumeujaalia kwa watu kuwa ni sawasawa; kwa wakaao humo na wageni. Na yeyote anayekusudia humo kufanya upotofu kwa dhulma Tutamuonjesha adhabu iumizayo.” (22:25)

Haijuzu kuchukua picha sawa kwenye msikiti mtakatifu wa Makkah wala kwenginepo. Lakini hata hivyo kwenye msikiti mtakatifu wa Makkah ni kubaya zaidi – tunaomba Allaah atukinge.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13379
  • Imechapishwa: 29/04/2018