Nasaha kwa wanaume wenye kuburuta nguo na wakataji ndevu


Swali: Tunaomba uwape nasaha kwa wale wanaochukulia wepesi au wanapunguza au kuzinyoa ndevu zao au kuvaa nguo zinazovuka kongo mbili za miguu hii leo?

Jibu: Tunawanasihi kutendea kazi Sunnah:

“Zirefusheni ndevu na punguzeni masharubu… “

Hii ndio nasaha. Tunamnasihi yale aliyoamrishwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Fugeni ndevu… “

“Ziacheni ndevu… “

“Zirefusheni ndevu na punguzeni masharubu… “

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqiyqatu Da´wat-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17206
  • Imechapishwa: 28/01/2018