Nasaha kwa wanaopenda vikao kama vya kahawa na vijiweni


Swali: Baadhi ya watu sehemu za kustarehe na katika vikao hawajichungi kutokamana na upuuzi mwingi, maneno mengi na mizaha mingi. Ni mamoja hayo yakawa ya kweli au ya uongo. Unawanasihi nini?

Jibu: Nawanasihi kutomsahau kumtaja Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika vikao vyao. Wanapotaka kusimama na kuondoka zao basi wasome kafara ya kikao:

سُبحانك اللهم وبِحمدك أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوبُ إِلَيْك

“Utakasifu ni Wako, ee Allaah, kutokamana na mapungufu, himdi zote unastahiki Wewe, nakuomba msamaha na kutubia Kwako.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16857
  • Imechapishwa: 17/03/2018