Swali 743: Mimi ni mwanamke mtiifu kwa mume wangu na nimefungamana na maamrisho ya Allaah. Lakini sikutani naye kwa furaha na kwa uso wenye tabasamu. Hilo ni kwa sababu hatimizi zile haki ambazo ni wajibu kwake kama vile mavazi. Nimemuhama kitandani. Je, ninapata dhambi kwa kitendo hicho?

Jibu: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewajibisha kutangamana kwa wema baina ya mke na mume na kila mmoja atekeleze kile kinachomuwajibikia. Lengo ni manufaa na maslahi ya kindoa yaweze kutimia. Ni lazima kwa mume na mke kila mmoja katika wao awe na uvumilivu juu ya yale mapungufu na matangamano maovu anayoyapata kutoka kwa mwengine. Mume anatakiwa kutekeleza yale yanayomlazimu na amuombe Allaah zile haki zake. Kufanya hivo ni miongoni mwa sababu za familia kubaki, kusadiana na ndoa kubaki.

Dada muulizaji nakunasihi kusubiri juu ya yale mapungufu unayokutana nayo kutoka kwa mume wako na utekeleze zile haki za kindoa zinazokuwajibikia. Kwani hakika mwisho – kwa idhini ya Allaah – huwa mzuri. Pengine kule kusimamia wajibu wako kukamfanya akabadilika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 290
  • Imechapishwa: 07/10/2019