Nasaha kwa wanafunzi juu ya kuamrisha mema na kukemea maovu

Swali: Nataraji utawahimiza wanafunzi juu ya jambo la kuamrisha mema na kukataza maovu kwa sababu maovu yamekithiri na kwa hivyo ni lazima kuwahimiza watu juu ya hilo?

Jibu: Ni lazima kusaidiana. Amesema (Ta´ala):

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

“Saidianeni katika wema na uchaji Allaah, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui.” (05:02)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule katika nyinyi atakayeona maovu, basi ayakemee kwa mkono wake. Asipoweza, afanye hivo kwa ulimi wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa moyo wake – na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”[1]

Kukemea kunakuwa kwa mikono kwa yule anayeweza kama watawala na mtu nyumbani kwake. Kuhusu ambaye hawezi na wakati huohuo akawa anajua hukumu ya uovu huu, basi akataze kwa kutoa nasaha na kubainisha. Ikiwa pia hilo hawezi na linapelekea katika madhara, basi akemee kwa moyo wake. Kwa msemo mwingine ni kwamba anatakiwa kukemea maovu hayo na kujitenga na mahali hapo.

[1] Muslim (49).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (07) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/434/434.mp3
  • Imechapishwa: 05/04/2019