Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Himdi zote anastahiki Allaah. Swalah na salaam zimwendee Mtume wa Allaah, ahli zake, Maswahabah zake na atakayefuata uongofu wake. Amma ba´d:

Imeenea kupitia vyombo vya khabari ya kuwa Papa wa Vatican Benedict XVI ameutukana Uislamu na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kitendo kama hicho ni cha ajabu na kinapingana na mantiki, akili timamu na uhakika, sura safi ya Uislamu.

Kwa Uislamu huu Allaah amemuokoa mwanaadamu kutoka katika Uislamu kwenda katika mwanga. Amemuokoa kutoka katika dini za kijeuri na kwenda katika uadilifu wa Uislamu ambao umeshuhudiwa na maadui werevu. Sintorefusha juu ya kusifu Uislamu na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu umeueneza na kuupamba ulimwengu kwa kheri na kuzipamba maktabah. Hivyo nitafupisha na kusema:

Hakika Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Mtume wa Allaah wa haki na wa kweli. Allaah amemtuma akiwa ni rehema kwa walimwengu. Amemtuma akiwa ni mwenye kutoa bishara njema na kuonya, akilingania katika Uislamu na taa lenye kuangaza. Ujumbe wake ni wenye kuwaheshimu Manabii na vitabu vyao. Bali ujumbe wake una kuwapenda na kuwaamini na vitabu vyao. Allaah (Ta´ala) amesema:

آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ

“Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake na Waumini. Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Mtume Wake.” (02:285)

Allaah (Ta´ala) amesema akimwamrisha Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Ummah wake waseme:

قُولُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَا أُوتِيَ النَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ

“Semeni: “Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na al-Asbaatw na aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na waliyopewa Manabii kutoka kwa Mola wao – hatutofautishi baina ya mmoja yeyote miongoni mwao nasi Kwake tunajisalimisha.” (02:136)

قُلْ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ عَلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَالنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ

“Sema: “Tumemwamini Allaah, na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym, na Ismaa’iyl na Is-haaq, na Ya’quwb na al-Asbaatw na yale aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na Manabii kutoka kwa Mola wao – hatutofautishi baina ya mmoja yeyote miongoni mwao, nasi Kwake tumejisalimisha.” (03:84)

Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekuja kwa uadilifu na wema. Amekataza machafu na madhambi:

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ

“Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na wemaa na kuwapa [mahitajio na msaada] jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na maovu na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumbuka.” (16:90)

Ujumbe wake umekuja kwa Jihaad ili kulinyanyua neno la Allaah liweze kuwa juu na kutokomeza kufuru, shirki na ufisadi. Hapo kabla Muusa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) na Manabii wengine wa wana wa Israaiyl baada yake walimtangulia kuja na ujumbe kama huo.

Ujumbe wake una kisasi na adhabu zilizowekwa katika Shari´ah kwa ajili ya kuhifadhi dini, nafsi, heshima na mali. Hapo kabla Muusa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) na Manabii wengine wa wana wa Israaiyl baada yake walimtangulia kuja na ujumbe kama huo.

Ujumbe huu una kheri, wema na kuzilinda heshima na mali. Hali kadhalika unafanya kuwepo kwa amani na uaminifu, kuleta manufaa na kuzuia madhara.

Hakuna mwenye kumsifu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ujumbe wake kwa njia mbaya isipokuwa aliye muongo na kafiri ambaye wakati huo huo ni mwenye kumtukana pia Muusa, ujumbe wake na Manabii wa wana wa Israaiyl baada yake ambao walikuwa wakihukumu kwa Tawraat. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّا أَنزَلْنَا التَّوْرَاةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ ۚ يَحْكُمُ بِهَا النَّبِيُّونَ الَّذِينَ أَسْلَمُوا لِلَّذِينَ هَادُوا وَالرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ بِمَا اسْتُحْفِظُوا مِن كِتَابِ اللَّـهِ وَكَانُوا عَلَيْهِ شُهَدَاءَ ۚ فَلَا تَخْشَوُا النَّاسَ وَاخْشَوْنِ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ وَكَتَبْنَا عَلَيْهِمْ فِيهَا أَنَّ النَّفْسَ بِالنَّفْسِ وَالْعَيْنَ بِالْعَيْنِ وَالْأَنفَ بِالْأَنفِ وَالْأُذُنَ بِالْأُذُنِ وَالسِّنَّ بِالسِّنِّ وَالْجُرُوحَ قِصَاصٌ ۚ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِ فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَّهُ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ

“Hakika Tumeteremsha Tawraat humo mna mwongozo na nuru; ambayo kwayo, Manabii waliojisalimisha, wanavyuoni wafanyao mno ‘ibaadah na kufanyia kazi elimu zao na marabi waliwahukumu Mayahudi, kwani walikabidhiwa kukihifadhi Kitabu cha Allaah. Nao wakawa mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali Niogopeni. Na wala msibadili Aayaat Zangu kwa thamani ndogo. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri. Na humo Tumewaandikia ya kwamba uhai kwa uhai, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, jino kwa jino na majaraha [kulipizana] kisasi. Lakini atakayetolea swadaqah [haki yake akasemehe] kwayo, basi itakuwa ni kafara kwake. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu. (05:44-45)

وَلْيَحْكُمْ أَهْلُ الْإِنجِيلِ بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فِيهِ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ

“Na watu [waliopewa] Injiyl wahukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah ndani yake. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki.” (05:47)

Mayahudi na manaswara wote wawili wameikufuru Tawraat na Injiyl na matokeo yake hawakutendea kazi I´tiqaad na hukumu zilizomo humo. Wamemkadhibisha Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amewajia akiwasadikisha Mitume na vitabu, ikiwa ni pamoja vilevile na Tawraat na Injiyl. Wamemkufuru Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ujumbe wake wenye kuwasadikisha Mitume wote na zile I´tiqaad na hukumu zilizomo katika Tawraat na Injiyl. Kunavuliwa tu yale ambayo yamefutwa na Uislamu.

Kwa kiburi, kuchukia haki na hasadi wakampiga vita na khaswa marabi, watawa na mapapa wao baada ya kupotosha vitabu vyao, kucheza na maandiko yake na wakafanya I´tiqaad zao; Tawhiyd na mani kuwa ni shirki na kufuru, wakakanusha hukumu zilizomo ndani yake.

Ikiwa huu ndio msimamo wao kwa vitabu ambavyo wanasema kuwa wanaviamini, vipi watakuwa na uzito wa kumkufuru Muhammad (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Qur-aan isiyoingiliwa na batili kati yake wala nyuma yake?

Mayahudi na manaswara! Tubuni kwa Allaah tawbah ya kweli na mfuateni Muhammad ambaye amebashiriwa na vitabu vyenu. ´Iysaa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) amebashiria juu yake na kusema:

وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُم بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ

“Na ‘Iysaa mwana wa Maryam aliposema: “Enyi wana wa Israaiyl! Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat na mwenye kubashiria kuja kwa Mtume baada yangu jina lake: Ahmad.” Basi alipowajia kwa hoja bayana, walisema: “Huu ni uchawi wa wazi”.” (61:06)

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ

“Sema: “Enyi Ahl-ul-Kitaab! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, kwamba: tusiabudu isipokuwa Allaah Pekee, na wala tusimshirikishe na chochote, na wala wasichukue baadhi yetu wengine [wakawafanya] waungu badala ya Allaah.” Wakikengeuka; basi semeni: “Shuhudieni kwamba sisi ni Waislamu”.” (03:64)

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَلْبِسُونَ الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

“Enyi Ahl-ul-Kitaab! Kwanini mnachanganya haki na batili na mnaficha haki na hali nyinyi mnajua?” (03:71)

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ مَنْ آمَنَ تَبْغُونَهَا عِوَجًا وَأَنتُمْ شُهَدَاءُ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ

“Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! Kwanini mnamzuilia aliyeamini njia ya Allaah mnaitafutia upotofu na hali nyinyi mashahidi? Na Allaah si Mwenye kughafilika kwa myatendayo.” (03:99)

Wewe unayeitwa Papa wa Vatican! Kuwa muislamu, utasalimika! Allaah atakupa ujira mara mbili. Ukikataa, basi utabeba madhambi ya wafuasi wako manaswara wote. Kuwa muislamu na wasilimu vilevile wenzako wa dini moja kama wewe. Mkifanya hivo, basi Allaah atakuingizeni katika Pepo ambayo ukubwa wake ni kama mbingu na ardhi ambayo imeandaliwa kwa ajili ya wamchao Allaah, wafuasi wa Mitume wa kweli. Amini Qur-aan hii kubwa ambayo imezishinda nyujumbe zingine zote. Imekuja kwa I´tiqaad sahihi na hukumu adilifu zinazosapotiwa na akili timamu na maumbile yaliyosalimika. Amini, wewe na wafuasi wako, Qur-aan hii ilio na yale niliyokutajieni na ina sifa za kipekee na miujiza.

Allaah aliwapa changamoto majini na wanaadamu walete mfano wake. Wakashindwa bali hawakuweza kuleta Suurah kumi mfano wake ijapokuwa Suurah moja tu. Wameshindwa wakashindwa wakashindwa, hata kama watakuwa ni wenye kusaidizana kati hayo.

Lau mapapa na wafuasi wao wangelikuwa na akili ijapokuwa kidogo, uelewa na uadilifu, basi haya yangetosheleza kwao kuiamini.

Mapapa! Kuweni waislamu mtasalimika. Mkifanya hivo, mtapata Pepo ambayo ukubwa wake ni kama mbngu na ardhi. Msipofanya hivyo, basi kuweni na yakini ya kupata adhabu kali na ya milele katika Moto ambao Allaah ameundaa kwa ajili ya makafiri. Joto lake ni kali na rindi lake ni refu. Allaah (Ta´ala) amesema katika Qur-aan tukufu na Kitabu Chake chenye hekima:

إِنَّا أَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ سَلَاسِلَ وَأَغْلَالًا وَسَعِيرًا

“Hakika Sisi Tumewaandalia makafiri minyororo, na pingu na [Moto wa] Sa’iyraa.” (76:04)

وَذَرْنِي وَالْمُكَذِّبِينَ أُولِي النَّعْمَةِ وَمَهِّلْهُمْ قَلِيلًا إِنَّ لَدَيْنَا أَنكَالًا وَجَحِيمًا وَطَعَامًا ذَا غُصَّةٍ وَعَذَابًا أَلِيمًا يَوْمَ تَرْجُفُ الْأَرْضُ وَالْجِبَالُ وَكَانَتِ الْجِبَالُ كَثِيبًا مَّهِيلًا

“Na Niache Mimi na wanaokadhibisha walioneemeka na uwape muhula kidogo. Hakika Sisi Tuna minyororo na [Moto wa] Jahiymaah, na chakula cha kukwama kooni, na adhabu iumizayo. Siku itakayotikisika ardhi na majabali na majabali yatakuwa kama chungu ya mchanga unaporomoka.” (73:11-14)

Mapapa! Msidanganyike na uhai wa duniani. Tambueni kuwa waliokuwa kabla yenu walipotosha vitabu vyene, kuharibu dini yenu na wakawafanya watu kuwa miungu badala ya Allaah. Wakadai kuwa ´Iysaa ni mwana wa Allaah au imani ya utatu – Allaah ametakasika na hayo. Allaah (Ta´ala) amesema katika Kitabu Chake cha milele na cha miujiza kilicholindwa na upotoshaji na mabadiliko:

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ اللَّـهُ الصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

“Sema: “Yeye ndiye Allaah wa Mmoja Pekee. Allaah Mwenye kukusudiwa. Hakuzaa na wala Hakuzaliwa. Na hana anayefanana [au kulingana] Naye.” (112:01-04)

لَّقَدْ جِئْتُمْ شَيْئًا إِدًّا تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الْأَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدًّا أَن دَعَوْا لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدًا وَمَا يَنبَغِي لِلرَّحْمَـٰنِ أَن يَتَّخِذَ وَلَدًا إِن كُلُّ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ إِلَّا آتِي الرَّحْمَـٰنِ عَبْدًا لَّقَدْ أَحْصَاهُمْ وَعَدَّهُمْ عَدًّا وَكُلُّهُمْ آتِيهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَرْدًا

“Hakika mmeleta jambo ovu mno! Zinakaribia mbingu ziraruke [kwa tamko] hilo, na ardhi kupasuka, na majabali kuporomoka na kubomoka. Kwa kule kudai kuwa Mwingi wa Rahmah ana mwana. Na wala haiwii [wala haielekei kabisa] kwa Mwingi wa Rahmah kujichukulia mwana. Hakuna yeyote [yule aliyomo] katika mbingu na ardhi isipokuwa [Siku ya kufufuliwa] atamfikia Mwingi wa Rahmah akiwa ni mja. Kwa hakika Amewarekodi barabarana Amewahesabu [hesabu ya] sawasawa. Na kila mmoja katika wao atamfikia Siku ya Qiyaamah akiwa pekee.” (19:89-95)

Mayahudi na manaswara! Mapapa! Mitume wote walikuja kufikisha Tawhiyd na kupiga vita shirki. Miongoni mwao ni pamoja vilevile na ´Iysaa (´alayhis-Swalaatu was-Saalam):

لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ

“Kwa hakika wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni al-Masiyh mwana wa Maryam.” Na al-Masiyh alisema: “Enyi wana wa Israaiyl! Mwabuduni Allaah, Mola wangu na Mola wenu. Kwani hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Pepo, na makazi yake yatakuwa ni Motoni. Na madhalimu hawatopata mwenye kunusuru yeyote!” (05:72)

Hakika (´alayhis-Salaam) aliamrisha kumuabudu Allaah peke yake. Alisema wazi wazi ya kwamba Allaah ndiye Mola Wake na Mola wa aliotumilizwa kwao. Amesema yule mwenye kumshirikisha Allaah basi ataingia Motoni. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

“Kwa hakika wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni watatu wa utatu.” Ilihali hakuna mungu wa haki isipokuwa Mmoja Pekee. Na wasipoacha yale wanayoyasema, bila ya shaka itawagusa wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo.” (05:73)

Manaswara na mapapa! Komeni na yale Allaah aliyokutahadharisheni; kumuabudu ´Iysaa na viumbe wengine! Endapo mtafanya hivo, basi nyinyi mko katika kufuru na shirki. Malipo ya hilo Allaah atakuharamishieni Pepo na atafanya mafikio yenu ni Motoni.

Msidanganyike na mababu zenu, mapapa na watawa. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba hawafuati jengine isipokuwa batili na kufuru. Nimeshatangulia kukwambieni kuwa walipotosha Tawraat na Injiyl.

Msidhani kuwa ´Iysaa atakushufaeni au kukuingizeni Peponi na kukusalimisheni na Moto. Hili haliko mikononi mwake. Mmetofautiana naye, ´Aqiydah yake na ´Aqiydah ya Tawhiyd. Mmemfanya kuwa ni mungu ilihali anamkufurisha mwenye kufanya hivo. Atawakaneni nyinyi pamoja na upotevu wenu na kule kumfanya yeye na mama yake kuwa ni waungu badala ya Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـٰهَيْنِ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالَ سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ ۚ إِن كُنتُ قُلْتُهُ فَقَدْ عَلِمْتَهُ ۚ تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ ۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ مَا قُلْتُ لَهُمْ إِلَّا مَا أَمَرْتَنِي بِهِ أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۚ وَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ

“Na Allaah Atakaposema: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Je, wewe uliwaambia watu: “Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu miwili badala ya Allaah?” Atasema: “Utakasifu ni Wako! Hainipasi mimi kusema yasiyo kuwa haki kwangu; ikiwa nimesema hayo basi kwa yakini Ungeliyajua – Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu na wala mimi sijui yale yaliyomo katika Nafsi Yako. Hakika Wewe ni Mjuzi wa ghayb. Sijawaambia lolote ila yale Uliyoniamrisha kwayo kwamba: Mwabuduni Allaah Mola wangu na Mola wenu. Na nilikuwa juu yao shahidi wakati nilipokuwa nao. Uliponichukua juu [mbinguni] Ulikuwa Wewe Mwenye kuchunga juu yao na Wewe juu ya kila kitu ni Mwenye kushuhudia. Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni waja Wako; na Ukiwasamehe basi hakika Wewe ni Mwenye nguvu kabisa, Mwenye hikmah wa yote. (05:116-118)

´Iysaa anakana ´Aqiydah ya kinaswara batili juu yake na juu ya mama yake ya kwamba wao ni waungu. Atamwambia Allaah ya kwamba hakuwaamrisha watu jengine isipokuwa kile Mola Wake alichomuamrisha: kumuabuu Allaah, Mola Wake na Mola Wao.

Mkikanusha haki iliyomo ndani ya barua hii na mkaendelea kuleta ubishi na majadiliano, basi ninakuiteni kufanya maapizano kama ambavyo Allaah alivyomuamrisha Mtume Wake wa haki na wa kweli. Alimwambia:

فَمَنْ حَاجَّكَ فِيهِ مِن بَعْدِ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ فَقُلْ تَعَالَوْا نَدْعُ أَبْنَاءَنَا وَأَبْنَاءَكُمْ وَنِسَاءَنَا وَنِسَاءَكُمْ وَأَنفُسَنَا وَأَنفُسَكُمْ ثُمَّ نَبْتَهِلْ فَنَجْعَل لَّعْنَتَ اللَّـهِ عَلَى الْكَاذِبِينَ

“Basi yeyote atakayekuhoji kwayo baada ya kukujia elimu, basi sema: “Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu, na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu, tuifanye laana ya Allaah iwe juu ya waongo [kati yetu].” (03:61)

Mimi na kila muislamu tuna kiigizo chema kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Amani iwe juu ya yule mwenye kufuata uongofu.

Imeandikwa na:

Rabiy´ bin Haadiy ´Umayr al-Madkhaliy
24/Sha´baan/1427

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy ´Umayr al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=153
  • Imechapishwa: 30/04/2020