Swali: Kuna mtu anapoenda chooni kwa ajili ya kutawadha basi hubaki huko kwa muda mrefu. Baadhi ya nyakati, kama swalah ya Fajr, jua linachomoza ilihali bado hajamaliza kutawadha. Wakati nilipomuuliza sababu ya hilo akasema kwamba anahisi kuwa anatokwa na mkojo na kwamba anasubiri mkojo utoke wote na kwamba kila anapomaliza kutawadha basi anahisi kuwa ametokwa na mkojo mara nyingine. Je, inafaa kwake kusubiri mpaka pale mkojo utatoka wote pamoja na kwamba wakati wa swalah utatoka nje? Je, inajuzu kuzidisha kuosha viungo vya wuduu´ zaidi ya mara tatu?

Jibu: Tunamuomba Allaah amponye. Ee Allaah! Mponye! Haya ni maradhi. Ni maradhi yanayoitwa ´wasiwasi`. Namwambia hali ya kuwa ni nasaha kwake, pale atapojiambia mwenyewe kwa mara ya kwanza kwamba mkojo umeshatoka wote, basi ajisafishe kwa maji kisha atawadhe na aende zake kuswali. Ama ukibaki basi shaytwaan atakuchezea, atazuia mkojo hapa na hapa mpaka amshawishi. Nataraji atazinduka juu ya hili. Pale tu anapomaliza kukojoa basi ajisafishe kwa maji, atawadhe na kwenda zake kuswali. Utapozowea kufanya hivi basi Allaah atakuondoshea kile kilichokupata.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (62) http://binothaimeen.net/content/1420
  • Imechapishwa: 24/12/2019