Nasaha kwa mwenye kupenda kusema sana


Swali: Muulizaji huyu anaomba nasaha ya kuacha kusema sana.

Jibu: Ina maana anasema sana? Dawa yake ni kumdhukuru Allaah sana (´Azza wa Jall) na aache kusema sana na kuropokwa maneno yasiyokuwa na faida au yana shari. Achunge ulimi wake. Ulimi wako unaumiliki wewe na unaweza kuuchunga. Asiyeweza kuchunga ulimi wake ima ni mwendawazimu au aliyeumbwa pasina kuwa na akili. Ama mtu mwenye akili ambaye Allaah Amemtunukia akili, anauchunga ulimi wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (49) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-5-13.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014