Nasaha kwa mwanamke mchaji asiyemtii mume wake

Swali: Mke wangu anaswali Nawaafil nyingi za swawm, swalah na kusoma Qur-aan. Lakini hata hivyo hajihimizi kumtii mume wake na khaswa upande wa kitandani. Naomba umnasihi.

Jibu: Ninamnasihi mke wake kumtii mume wake kwa kuwa ni katika kumtii Allaah. Atekeleze haki zake na asimuasi katika wema. Atekeleze maombi yake kwa kuwa hili ni katika kumtii Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema katika Hadiyth Swahiyh:

“Mwanamke akiswali vitano vyake, akafunga mwezi wake, akamtii mume wake na akahifadhi tupu yake, basi ataambiwa [siku ya Qiyaamah]: “Ingia Peponi kwa mlango wowote unaoutaka.””

Mwanamke huyu amefanya mapungufu katika haki za mume wake. Hivyo kunakhofiwa juu yake asipate hili. Ninamnasihi mwanamke huyu atubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) na atekeleze haki za mume wake na asichelewe kumtekelezea maombi yake. Amtii katika mema.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://shrajhi.com//Live/ArID/339
  • Imechapishwa: 19/09/2020